JE UNA KIPARA? RONALDO ANA DAWA YA VIPARA KWA WANAUME.

0

Mchezaji soka maarufu duniani Cristiano Ronaldo amefungua kliniki yake ya kibiashara inayojihusha na kutibu vipara kwa wanaume kupitia upandikizi wa nywele na upasuaji.

Akizundua rasmi kliniki hiyo nchini Uhispania, Ronaldo akiwa ameandamana na mkwewe Georgina Rodriguez, alisema aliamua kufungua kliniki hiyo kuwapa uwezo wanaume kuthibiti muonekano wao katika jamii.

Kiliniki hiyo ya kisasa itatibu vipara kwa wanaume kupitia upandikizi wa nywele kichwani na pia itatoa huduma za upandikizi wa kope na nyusi kwa wanawake.

Hata hivyo Ronaldo mwenye miaka 34 amekana kwamba amewahikupata mataibabu ya kipara, akieleza kuwa nywele alizonazo kwa sasa ni zake asilimia 100%.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar