JE, NI KWELI FID Q AMEMLENGA JOH MAKINI KATIKA WIMBO “KIBERITI”

0

Rapa Fid Q wa nchini Tanzania amepinga uvumi kwamba baadhi ya mistari katika wimbo wake mpya kwa jina kibiriti aliomshirikisha Saida Karoli inamlenga rapa Joh Makini.

Rapa Fid Q anasema wimbo huo haumhusu msanii yeyote mwengine na kufichua kuwa mistari hiyo inaongelea maisha yake kama msanii.

Hata hivyo Fid Q amekiri kwamba baadhi ya mistari inawalenga watu ambao siku za karibuni wamekua wakimponda kuhusiana na kazi zake mpya.

Fid Q ameeleza kua dhana ya uwepo wa uhasama baina yao inaletwa na mashabiki wa Hip Hop kumlinganisha yeye na Joh Makini, kutokana na kazi zao nzuri, toka walipoanza kufanya mziki wa Hip Hop.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar