JE NI KWELI DOGO JANJA AMEFUNGA NDOA NA IRENE UWOYA?

0

Mama mzazi wa msanii Dogo Janja wa nchin Tanzania Bi. Zaituni Omari, amethibitsha kwamba taarifa za mtoto wake kufunga ndoa na Irene Uwoya ni za kweli.

Bi. Zaituni anasema  yeye kama mzazi alimpa baraka zote Dogo Janja kumuoa Irene Uwoya.

Kuhusu suala la tofauti ya umri kati ya mwanawe Dogo Janja na Irene Uwoya, mama Dogo Janja amesema kwamba suala la umri halijalishi sana kikubwa ni maelewano.

Dogo Janja ana umri wa miaka ishirini na mbili (22) na Mrembo Uwoya anadaiwa kuwa na umri wa miaka ishirini na tisa (29)

“Nimeridhika kwa sababu hata dini yetu ya Kiislam Mtume Mohamad alioa mwanamke mkubwa, kwa hiyo umri haujalishi, kikubwa na maelewano”, amesema mama yake Dogo Janja.

Ijumaa ya wiki iliyopita kulianza kuonekana kwa picha mtandaoni zinazoonyesha Irene Uwoya na Dogo Janja lakinimwenyewe amesalia kimya na hajazungumzia taarifa hizi

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar