JE BELLE 9 ANAHAMIA WASAFI (WCB)?

0

Baada ya vocalist, Rich Mavoko kusaini WCB ya Diamond, huwenda msanii mwengine wa wa R&B nchini humo Belle 9 akasaini ndani ya label hiyo pia.

Kulingana na taarifa nchini humo, Belle 9 anayefanya vizuri na wimbo ‘Bugger Movie Selfie’ ameonekana akifanya mazoezi ya bendi ya Diamond katika ofisi za WCB.

Aidha Belle pamoja na Diamond wameonekana wakiimba wimbo ‘Mdogo Mdogo’ kwa pamoja huku wakicheza, hatua iliyofufua uvumi kwamba huenda Belle 9 akafuata nyayo za za Rich Mavoko na kujiunga na WCB.

Kwa sasa label ya WCB ina wasanii wanne, Harmonize, Rich Mavoko, Raymond aka Rayvany pamoja Queen Darlin.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar