JAGUAR AZUNGUMZIA UVUMI WA KUPATA AJALI

0

Charles Njagua Kanyi a.k.a Jaguar amejipat katika hali isiyokua ya kawaida, baada ya uvumi kusambaa kwamba alihusika katika ajali na kufariki.

Kulingana na uvumi uliokua ukisambaa katika mitandao ya kijamii, Jaguar alifariki katika ajali iliyohusisha gari aina ya Noah alokua akisafiria kwenye barabara kuu ya Nairobi-Nakuru.

jaguar2

Hata hivyo mapema jana Jaguar alijitokeza na kukanisha uvumi huu akidai ako salama salmini na wala hajahusika katika ajali yeyote.

“Habari marafiki, naomba nianze kwa kuomba radhi kwa wote ambao watakua wameumizwa na uvumi kuwa nimefariki kwa ajali ya gari,  naomba niwadhibitishie kuwa mimi ni mzima na naendelea vizuri na kazi zangu”  –Jaguar

Jaguar amewataka mashabiki kupuuza uvumi huu na pia kuomba radhi familia iliyohusika kwenye ajali iliyokua ikizungumziwa.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar