HERMONIZE AZUNGUMZIA MAISHA YAKE NA WOLPER

0

Msanii wa label ya WCB, Harmonize anasema kidogo anachokipata kutokana na kazi zake za muziki  lazima ahakikishe anakula na baby wake ili kulinda status yake.

Harmonize ambaye anatoka kimapenzi na staa wa filamu TZ, Jacqueline Wolper, anasema gharama za kumtunza mrembo huyo hazimsumbui kama watu wanavyofikiria.

“Suala la kinywaji vyumbani kwake ana kaunta,so akijisikia kunywa anakunywa nyumbani, mimi nirudi studio namkuta anakunywa, na hajawahi kuniambia sijui anatoka na mashoga zake,” amefunguka Harmonize.

Hat hivyo Hermonize ameweka wazi kwamba katika harakati za kumshughulikia baby wake, hawezi kumsahau mamake mzazi na kumtelekeza.

“ sidhani kama kuna mwanaume mjinga ambaye anaweza kutelekeza familia yake kwa ajili ya mwanamke, kwa sababu sidhani bila Mama yangu kunizaa na kunituza ningemjua mwanamke, so kwanza Mama yangu halafu inakuja familia yangu, na kwa sababu mwanamke wangu ni sehemu ya familia yangu,” alimalizia Hermonize.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar