HATIMAYE FID Q ANASWA KATIKA MAPENZI

0

Thugs get lonely too…!

Ni kauli ya rapper maarufu ulimwenguni Tupac Shakur akizungumzia nafasi ya mapenzi katika ulimwengu wa ma’rapper hardcore.

Mkali wa Hip Hop nchini Tanzania Fid Q hatimaye ameinua mikono na kukumbatia swala la mapenzi .

Fid Q amemtambulisha mwandada mmoja kwenye mtandao wa kijamii ambaye amethibitisha ako katika mahusioano ya kimapenzi naye.

Fid Q ambaye inadaiwa tayari amemtambulisha kwao msichana huyu, amesema ameamua kufichua kwa mashabiki hali yake ya kimapenzi kupunguza idadi ya wasichana wanao mtumia meseji za kumtaka kimapenzi na pia kuwaonyesha mashabiki kwamba kwa sasa yupo katika mahusiano rasmi kwani umri wake unaruhusu.

Fid Q ametoa tahadhari kwamba mda wowote kuanzia sasa anaweza kutangaza ndoa.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar