HARMONIZE AZUILIWA NA POLISI.

0

Msanii Bongo Fleva toka kundi la WCB, Harmonize alizuiliwa kwa zaidi ya masaa matano katika kituo kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam alipokwenda kujisalimisha baada ya kutuhumiwa kuvuta bangi alipokuwa nchini Ghana.

Harmonize alikua akiitikia wito wa mkuu wa jiji la Dar Es Salaam Paul Makonda, ambaye alimtaka akirudi nchini Tanzania achunguzwe kuhusiana na matumizi ya dawa za kulevya.

Tuhuma za uvutaji bangi zilizuka baada ya Harmonize kuonekana katika kipande cha video kinachosambaa katika mitandao ya kijamii akivuta kitu chenye moshi mwingi kinachodaiwa kuwa bangi.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar