DUBAI YA MKANA R.KELLY

0

Serikali ya Dubai imekanusha madai kwamba mkongwe wa RnB ulimwenguni R.Kelly amepangiwa show katika taifa hilo.

Dubai imetoa kauli hii baada ya R.Kelly kuitaka mahakama moja nchini Marekani kumpa ruhusa ya kusafiri hadi nchini Dubai kwa ajili ya kupiga show kwani imekua ngumu kwake kupata kazi nchini Marekani.

R.Kelly anakabiliwa na kesi ya unyanyasaji wa kimapenzi kwa wasichana chini ya umri wa miaka18 na kusafiri nje ya taifa hilo anahitaji ruhusa ya mahakama.

Serikali ya Dubai inasema hakuna klabu hata moja ambayo imemtafuta R.Kelly kwa ajili ya show.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar