DOGO RICHIE AZUNGUMZIA KIMYA CHAKE. JE MZIKI UMEMSHINDA PIA YEYE?

0

Ama kweli kimya kina mshindo!!!!!!!!

Baada ya msanii Dogo Richie kuteka tasnia ya mziki kanda ya pwani na kibao chake kwa jina “Mziki” ambacho aliskika akikejeli wasanii wenza kanda ya pwani waliokua wamenyamaza kwa mda mrefu, sasa hali imebadilika na pia yeye kasalia kimya kwa mda mrefu bila ya kutoa kazzi.

Kimya chake kimezua maswali mengi miongoni mwa mashabiki waliotaraijia ataendelea kutoa nyimbo mpya baada ya kipindi kifupi.

Hata hivyo hali imebadilika, sasa na baadhi ya wasanii aliowaimba katika kazi yake ya awali wamenza kunong’ona wakimulizia je, na yeye yuko wapi? Mbona Kimya ama pia yeye mziki umeshinda?

Akizungumzia tetesi hizi, Msanii Dogo Richie amekiri kusalia kimya kwa mda mrefu lakini amelezea sababu kuu ya kimya chake.

Dogo Richie ameeleza kua kwa sasa mamake ni mgonjwa na amejitwika jukumu la kumuuguza, jambo linalomfanya kuweka swala la mziki kando kwa mda, hadi mamake atakapo pata nafuu.

Dogo Richie amefichua kuwa kwa sasa kazi yake mpya iko tayari na anangoja tu wakati mwafaka wa kutoa kazi hiyo.

 

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar