DOGO JANJA AWASUTA WASANII WENZA TANZANIA

0

Rapa Dogo Janja kutoka nchini Tanzania anasema sasa hana imani na wasanii wenza nchini Tanzania.

Rapa huyu anasema sasa imejitokeza wazi kwamba wasanii nchini Tanzania wamekosa umoja hususan pale mmoja wao anapopatwa na tatizo.

Dogo Janja amefichua kuwa baadhi ya wasanii hufurahia masaibu ya wenzao na kuwatakia mabaya, ili waendelee kufaidi peke yao matunda ya tasnia ya mziki.

Dogo Janja amepiga mfano wa tukio la majuzi amabapo video ya utupu ya msanii wa kike Nandy ilivujishwa mtandaoni na kusambazwa.

Rapa huyu amefichua kuwa kuna baadhi ya wasanii walifurahia masaibu ya Nandy huku wakitaka baraza la sanaa nchin Tanzania BASATA limfungie kufuatia video hiyo ili na wao wapate show.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

SIHITAJI KIKI ZA KOLABO

Rapa Godzilla a.k.a King Zilla amesema hataki kolabo na mtu yoyote na taarifa ziwafikie kuwa kwa sasa anakuja na album mpya. Godzilla amefunguka na kusema ...
Skip to toolbar