DOGO JANJA AMCHANA YOUNG KILLER

0

Rapper Abdulazizi Chende a.k.a Dogo Janja a.k.a Janjaro kutoka nchini Tanzania amemchana msanii mwenzake katika tasnia ya bongo flavaz Erick Msodoki  a.k.a “Young Killer’.

Dogo Janja anadai Young Killer hawezi kufika popote kimziki bila uwepo wake katika Bongo Flavaz kwa sababu  atakosa kiki.

Dogo Janja anasema amemfuatilia Young Killer katika kazi zake za hivi karibuni na kugundua kuwa kabla ya kutoa ngoma, mpya ni lazima atafute kiki kupitia jina la Dogo Janja.

Dogo Janja anasema hatua hii ndio imemplekea yeye kumdharau Young Killer  kwani anamuona kama msanii ambaye anapenya kimziki kwa kutumia mgongo wake.

“Bila mimi yule bwana mdogo atakufa njaa, nimejaribu kumchunguza kila anapotaka kutoa ngoma mpya ni lazima atafute kiki kupitia mimi, iwe kwenye media ama kwenye mitandao ya kijamii, kwa hiyo kwa upande wangu naona jamaa hawezi kusimama mwenyewe,” amesema Dogo Janja.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar