DJ PINYE AMJIBU DNA.

0

Baada ya msanii DNA kutoa wimbo wa kumtusi DJ maarufu nchini DJ Pinye  kufuatia uhasama uliozuka majuzi, DJ Pinyeamejitokeza kumjibu msanii DNA.

Pinye amesema hababaishwi na hatua ya DNA kutoa wimbo wa kumtusi na kumkejili sababu ya msimamo wake kuhusu nyimbo mbovu anapoletewa na wasanii wachanga.

Pinye amesema katika safari yake ya kazi amekumbana na watu sampuli ya DNA ambao hawakufurahishwa na msmamo wake, lakini hilo halijawahi kumsimamisha katika kazi zake.

Pinye na DNA walikwaruzana baada ya Pinye kufichua kuwa amewahi kukataa kucheza nyimbo mbovu kutoka kwa wasanii wanaoenukia nakutaja mifano ambapo DNA na Khalligraph walihusika.

Khalligraph alichukulia kwa utani ufichuzi wa Pinye lakni DNA aliingia studio na kutoa wimbo wa kumtusi Pinye.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

NG’OMBE MJAMZITO AHUKUMIWA KIFO

Ng’ombe mmoja mjamzito kutoka nchi ya Bulgaria amehukumiwa kifo baada ya kuvuka mpaka wa nchi yake na kuelekea Serbia kinyume na sheria za wanyama nchini ...
Skip to toolbar