DIAMOND & ZARI WARUSHIANA MANENO MAZITO MITANDAONI.

0

Staa wa Bongo Flava, Diamond Platnumz na mzazi mwenzake Zari The Boss Lady wamerushiana maneno mazito kupitia akaunti zao za instagram kufuatia ushindi wa bao 3-0, wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ dhidi ya Uganda, siku Jumapili.

Diamond ndiye aliyeanza vita hivi baada ya Uganda kufungwa bao moja ambap ali’post ujumbe wa kejeli alioulekezea watu aliowaita wajombazake Tiffah (mwanawe) waliopo jiji la Kampala.

Diamond hakukomea hapo, baada ya mechi kukamilika ali’post ujumbe mwengine akiwaelekezea wagada ambapo alisema kama aliwafunga waganda magoli ya watoto bado walikua hawawezi kushindwa kuwafunga uwanjani katika mechi ya soka.

Zari ambaye ni Mganda na mamake Tiffah, alishindwa kuvumulia na kujibu kauli za Diamond kwa ku’ post msimamo wa jedwali la kufuzu likionyesha Uganda ikiongoza jedali hilo licha ya kupoteza mechi ya jumapili, ambapo aliwakumbusha watanzania kwamba kabla ya mechi hiyo kuchezwa, Uganda ilikua tayari imeshafuzu na mechi hiyo haikua na uzito wowote kwa Waganda.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar