MSANII DAVIDO AMPINGA RAIS WA NIGERIA!

0

Msanii mkubwa wa mziki nchini Nigeria amejitosa katika wimbi la siasa linaloendela kwa sasa nchini Nigeria, baada yakupinga hadharani agizo la rais la kuwataka watakaoshiriki kura kurudi nyumbani baada ya kupiga kura.

Davido amewataka vijana kusalia katika vituo vya upigaji kura pindi wanaposhiriki upigaji kura, ili kulinda kura zao.

Davido anaongoza list ndefu ya wasanii maarufu nchini Nigeria wanaogemea upande wa chama cha upinzani nchini Nigeria  PDP na kupinga chama tawala cha rais wa sasa Muhammadu Buhari (APC) ambaye pia anagombea tena urais.

Raia wa Nigeria wanatarajiwa kushiriki kura za uchaguzi mkuu wa taifa hilo tarehe 16 Februari.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar