DAVIDO AKUBALI KUMFANYIA HILI SHABIKI WAKE.

0

Msanii David Adeleke a.k.a Davido kutoka nchini Nigeria, amekubali kukutana na shabiki mmoja, ambaye siku chache zilizopita alitishia kujitoa uhai.

Shabiki huyu alitangaza atajiua ikifka Agosti tarehe13, ambayo ni siku yake ya kuzaliwa, endapo hatawza kukutana na Davido.

Shabiki huyu anadai tangu mwaka wa 2014, amejaribu kuwasiliana na Davido lakini hajawahi kufanikiwa kujibiwa wala kukutana na Davido.

Sasa Davido amekubali kukutana na shabiki huyu katika siku yake ya kuzaliwa.

Davido anasema yupo tayari kuhudhuria sherehe za birthday za shabiki huyu ili kuokoa maisha yake.

“Wiki chache zilizopita kulikuwa na video ya shabiki wangu akitangaza kujiua kutokana na kunitafuta kwa muda mrefu bila mafanikio ya kuniona, hivyo sipo tayari kusababisha kifo chake, nitahakikisha nakutana na naye siku yake ya kuzaliwa kwake ili niokoe maisha yake,” amesema  Davido kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar