CHAMELEONE AMCHANA SHEEBAH

0

Msanii mkubwa nchini Uganda Chameleone amemchana  hadharani msanii wa kike nchini Uganda Sheebah Karungi aka Queen Sheebah akimtaka kujifunza kuvaa vyema.

Chameleone amem’beza Sheebah kufuatia uhasama unaotokota kati ya kambi yake na kambi inayomsimia msanii Queen Sheebah ya TNS Camp.

Queen Sheebah

Uhasama baina ya Chamelone na TNS Camp umedhirika wazi baada ya tamasha moja ambalo wasanii wa Chameleone walikua wamepangiwa kutumbuiza kuahirishwa bila ya kutolewa kwa sababu za maana.

Chameleone aidha ameonya sheebah na kambi yake ya TNS kwamba hako tayari kuendeleza uhasama nao akidai ni aibu kwa msanii mzee kama Sheebah kushindana na wasanii chipkizi wa kambi yake.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar