BARAKA THE PRINCE ATIWA MBARONI. KISA?

0

Msanii wa muziki nchini Tanzania The Prince, anadaiwa kukamatwa na kuzuiliwa na polisi nchini Tanzania, kwa kile kilichodaiwa kama kumtapeli dada mmoja hela.

Katika kipande cha video kinachosambaa katika mitandao ya kijamii, Barakah The Prince anaonekana akibishana na maafisa wa polisi wa Tanzania waliokua wanamtia mbaroni kwa tuhuma za utapeli.

Taarifa zaidi nchini Tanzania ziaeleza  kuwa dada mhusika katika sakata hiyo ya utapeli amedai kuwa alimpa Barakah The Prince shilingi milioni tano za kitanzania, ambazo ni sawa na zaidi ya shilingi  laki mbili pesa za Kenya, kwa makubaliano kwamba angefanya mapenzi naye, lakini baadae alimgeuka na kutumia hela hizo kujinunulia gari.

Msichina huyo anadai Barakah alimwambia kuwa hangeweza kushiriki naye mapenzi sababu kwa sasa anampenzi anayempenda sana kwa jina Naj.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

RICK ROSS ATIMIZA HILI MAISHANI

Rapa maarufu nchini Marekani, Rick Ross, amepanua familia yake baada ya kupata mtoto mwengine. Rick Ross sasa ni baba wa mtoto wa kiume aliyempa jina ...
Skip to toolbar