BABU TALE WA “WASAFI” AWAKEJELI WAKENYA KUHUSU -“#PLAYKENYANMUSIC”

0

Meneja mmoja wa wasanii wa Record Label ya Wasafi inayomilikiwa na Diamond Platnmuz kutoka inchini Tanzania amewakejeli wasanii na mashabiki wa mziki kutoka Kenya, kuhusiana na kampein yao ya mitandao ya kijamii, ya kushinikiza mziki wa wasanii wa Kenya kupewa nafasi kubwa katika vituo vya televisheni na radio nchini Kenya.

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram, Babu Tale amewataka wasanii wa Wakenya na baadhi ya mashabiki wao kutolalamika kuhusiana na swala la mziki wa Tanzania kutawala stesheni za taifa lao, kwani miaka ya nyuma pia Tanzania ilikubali sana mziki kutoka mataifa jirani kuwatawala.

Akijipiga kifua Babu Tale, ameeleza kuwa Tanzania inatoa wasanii wapya kila baada ya kipindi kifupi na kuwataka Wakenya kuwacha kulalamikia utawala wa mziki wa Bongo Flava inchini Kenya na kupiga kazi.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

MCHEZAJI TAJIRI ZAIDI DUNIANI 2018

Bondia wa nchini Marekani, Floyd Mayweather ametwaa tena nafasi ya kwanza kwenye orodha ya wanamichezo 100 matajiri zaidi duniani kwa mujibu wa Jarida la kibiashara ...
Skip to toolbar