BAADA YA DIAMOND SASA MWANA FA. AMKATAA BABAKE MZAZI. KISA?

0

Mwanamuziki Khamis Mwinjuma maarufu Mwana Fa kutoka nchini Tanzania anaripotiwa kumkana babake mzazi licha ya kumfahamu.

Inasemkana Mwana Fa amekataa katakata kumtambua kwa hali na mali mzee moja kwa jina Mohammed Mazingazinga Mwinjuma ambaye ushahidi upo kwamba ndiye babake mzazi.

Imeelezwa kuwa Mwana Fa amekua akimkana na kutomsaidia mzee Mazingazinga baada ya mzee huyo kumtelekeza alipokua mdogo na kumuacha kulelewa na mamake.

Inadaiwa mzee Mazingazinga alihamia jijini Nairobi kwa shughuli za muziki na kusahau malezi ya Mwana Fa jambo ambalo msanii huyu ameshikilia kama sababu kuu ya kutomtambua mzee Mazingazinga

Aidha baada ya mamake mzazi Mwana Fa kufariki mzee Mazingazinga alioa mwanamke mwingine na kupata watoto ambao pia Mwana Fa amewakataa kwa madai sio wadogo zake.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar