AVRIL AMJIBU A.T. KUHUSU UWEZO WAKE WA KUIMBA

0

Msanii wa kike kutoka jijini Nairobi amejitokeza kuzungumzia kauli ya msanii mmoja wa nchini Tanzania kwa jina AT aliyebeza uwezo wake wa kuimba.

Mapema wiki iliyopita, msanii AT alinukuliwa na vyombo vya habari nchini Tanzania akidai msani Avril kutoka Kenya hajui kuimba.

Akijibu kauli ya AT msanii Avril amesema haoni haja ya kujibizana na msanii AT kwani hata yeye hamfahamu.

Avril aidha amekanusha madai ya TA kwamba waliwahi kukutana mwaka wa 2010 wakati msanii AT alipozuru studio za Ogopa Djs jijini Nairobi kurekodi wimbo flani.

Avril anasema haoni haja ya kufuatilia na kujibizana na mtu ambaye hajulikani.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar