APIGWA MARUFUKU NA MAHAKAMA KUTOIMBA NYUMBANI KWAKE

0

Mwanamke mmoja nchini Uingereza amepigwa marufuku kutoimba akiwa katika nyumba yake na mahakama ya jimbo la Norwich nchini humo.

Bi. Heather Webb mwenye umri wa miaka 48, ameagizwa na mahakama ya kutoimba wala kucheza mziki kwa sauti ya juu akiwa nyumbani kwake, baada ya majirani zake kulalamikia sauti yake mbovu.

Majirani wameeleza mahakama hiyo kuwa wamelazimika kuvumilia kwa miaka nne kelele za Bi. Webb toka mwaka wa 2014 alipohamia eneo lao.

Inaripotiwa kabla ya amri ya mahakama majuzi, majirani walipiga ripoti mara kadhaa kwa polisi wakilalamikia tabia yake ya kuimba kwa sauti mbovu ya kuwakera.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar