AFUNGA NDOA NA WANAWAKE WAWILI, HARUSI MOJA !

0

Jamaa mmoja ameibua hisia za wivu miongoni mwa wanaume wenginchini baada ya kufanikiwa kufunga ndoa na wanawake wawili kwa mpigo katika sherehe moja ya harusi.

Tom Makui aka Junior Mako kutoka kaunti ya Kajiado, ameweka rekodi nchini kwa kufunga ndoa na warembo wawili kwa majina Elizabeth Silamoi and Joyce Tikoyian katika harusi ya kufana

Akizungumza baada ya kufunga ndoa na wake wake wawili pamoja, Junior Mako ameeleza kuwa sababu kuu iliyomfanya kuamua kuoa wanawake wawili kwa pamoja ni kudhihirisha uaminifu wake kwa wapenzi wote wawili.

Junior Mako amewashauri vijana wengine kuiga mfano wake na kuoa wapenzi zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja iwapo mtu atahisi anawapenda wote na kuwataka kutobagua michepuko kwa kuiacha wanapofunga ndoa.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar