AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUNYAMBA!

0

Mfanyakazi mmoja nchini Australia amefika mahakama ya rufaa nchini humo katika kesi dhiidi ya bosi wake ya madai ya kumbugudhi ofisini kwa kunyamba sana.

David Hingst ambaye alikuwa ofisa utawala katika mji wa Melbourne , anadai kuwa bosi wake wa zamani kwa jina Greg Short katika kampuni moja kwa jina Construction Engineering, alikuwa akinyamba  sana mbele yake, jambo ambalo kwa sasa linamsababishia msongo wa mawazo.

Hingst mwenye umri wa miaka 56 anadai kulipwa dola milioni 1.28.

Mwaka jana mwezi April mahakama kuu nchini Australia ilitupilia mbali kesi hiyo ikiamua kuwa kunyamba hakukua sawa na dhulma aina yeyote.

Hingst alieleza mahakama kwamba bosi wake alikua akishuta takriban mara tano hadi sita kwa siku akiwa karibu naye kwa njia ya kumdhalilisha.

Mahakama ya rufaa imesema itatoa hukumu yake Ijumaa, Machi 29.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar