HUYU NDIYE WA KULAUMIWA KUFUATIA KUJAA KWA MZIKI WA KIGENI KATIKA RADIO PLAYLIST ZETU PWANI.

0

Rafiki yangu mmoja jana alinitumia ujumbe wa siri kupitia whatsap. Mshikaji huyu ni mmoja wa washikadau wakuu katika sanaa ya pwani, mtengezaji maarufu wa mziki kanda ya pwani. Rafiki yangu alikua analalamikia jinsi alivyopanda matatu moja akielekea nje ya jiji la Mombasa na kuskia DjMix iliyosheheni nyimbo tupu za Yamoto Band.

Kulinganana jamaa huyu, jambo lililomkera zaidi ni kwamba DjMix hiyo ilipomaliza nyimbo za Yamoto Band, zilingia nyimbo za Ali Kiba, Diamond n.k Hadi alipoteremka matatu ile, huyu jamaa asema hakuskia DjMix yenye angalau wimbo mmoja unaovuma kutoka kwa wasanii wa kanda ya pwani.

Swali aliloniuliza kwa uchungu ni je ma producer wetu hawafanyi kazi ya kutosha kiasi cha kutoshobokewa na ma’Dj wa Kenya kama wanavyoshobokewa wasanii wa Tz? Nani wa kulaumiwa wakati mziki wa kigeni unateka soko la kimziki pwani na kupoteza kabisa kazi za wasanii wa kwetu.

Aliniuliza swali hili kwa uchungu. Licha ya kuendelea na shughuli zangu za siku, ukweli ni kwamba swali hili liliniuma na kunikera zaidi.Nilihisi ni kama anaelekeza kidole cha lawama kwa watangazji, kitu ambacho kimekua tabia ya wengi wanaokerwa na hali hii.

Kwa hasira na kutafuta suluhu kwa njia ya mkato, ningelifanya swala hili mjadala katika kipindi changu, lakini tayari show prep ilikuepo na sikutaka kumtatiza mtangazaji-mwenza tunaye shirikiana naye katika kipindi. Usiku nilijipata nimerudia vitabu na kupekua pekua kutafuta jibu kwa ugonjwa huu, nani wa kulaumiwa zaidi?

Leo nimejaribu kadri ya uwezo,tajriba na upeo wangu wa fikra kulichanganua swala hili na kutoa jibu tofauti na wengi wanavyopenda kufikiria.

who-is-to-blame-1a1Nani Wa Kulaumiwa?

Kwa mtazamo wangu, mtu wa kulaumiwa kwa tatizo hili ni msikilizaji. Ndio! Msikilizaji . katika ulimwengu wa tasnia ya radio, anayejiita shabiki wa mziki wa kizazi kipya ndiye wa kulaumiwa. Anayekwenda club na kucheza mziki wa kigeni unapochezwa na Dj ni wa kulaumiwa. Wewe uliye na mziki wa kigeni katika simu yako ni wa kulaumiwa.

Mskilizaji wa radio ndiye anyefaa kulaumiwa zaidi wakati playlist za vipindi vyetu vya radio zinasheheni mziki wa kigeni. Kulingana mpangilio wakazi za radio na utangazji kwa ujumla, kila anayezungumza nyuma ya bomba hutaka kuwa na wasikilizaji wengi zaidi. Na ili kuwa na wasikilizaji wengi, lazima upeane kile kitu watu wengi wanapenda zaidi. Ndio maana kwa sasa radio nyingi kanda ya pwani playlist zao zinakaribia kufanana, kama hazifanani shilingi kwa ya pili tayari. Na cha ajabu nyimbo zinazochezwa sana ni za kigeni. Watangazji si wa kulaumiwa hapa. Ushindani katika radio umefikia viwango ambavyo havijawahi kushuhudiwa katika historia ya tasnia ya matangazo ya radio pwani.

Competition21

Ushindani

Utagundua kwa sasa radio nyingi za kanda ya pwani zimebadili mpangilio wao wa vipindi, vituo vimebadilisha watangazaji, radio nyengine zimeji’rebrand mara kadhaa. Yote haya si kwa sababu ya kupenda kwao, bali hali imelazimu iwapo wanataka kupata faida na kusalia katika biashara. Hakuna mtangazji aliyetayari kufutwa kazi itakapo bainika kipindi chake kina wasikilizaji wachache.

Wengi wasilolijua ni kwamba zipo kampuni maalum za utafiti ambazo hufanya utafiti kuhusu umaarufu wa watangazji, vipindi na radio na kutoa ripoti kila baada ya miezi mitatu (mara nne kwa mwaka). Sasa ripoti za utafiti kutoka kwa kampuni hizi ndio hua ni msema ukweli kuhusu mishahara na mikataba ya watangazaji wengi.

Wamiliki wa vituo na kampuni zinazotaka kutangaza hukimbilia ripoti hizi, ili kujua wapi pa kuekeza pesa zao kwa matangazo ili yapate kusikika na wengi zaidi. Wakati kipindi chako kina wasikilizaji wachache kama mtangazaji, hupati matangazo na mwishowe utafutwa kazi sababu huletei faida kwa kampuni iliyokuajiri na kukupa nafasi ya kwenda hewani. Hapa ndio utapata watangazaji wengi wako tayari kufanya kila aina ya mbinu chafu na safi kuhakikisha wanasalia na wasikilizaji wengi. Miongoni mwa mbinu hizi ni kuhakikisha wanacheza mziki mzuri, unaojulikana na kupendwa na watu wengi zaidi wanaoskiliza radio.

Sasa hapa lawama kwa nani?

theory-wordle
Nadharia(Theory)

Ninacho sema hapa si kutetea watangazji bali ukweli ambao umeepuka upeo wa washikadau wengi wa tasnia. Upo ushahidi wa nadharia za wasomi zilizohakikishwa na kupitishwa na wasomi wa maswala ya mawasiliano na utangazji, zinaoonyesha kwamba msikilizaji na mtazamaji ndiye anayeamua kinachosikika kwenye radio na kuonekana kwenye tv.

Kulingana na nadharia moja maarufu miongoni mwa wasomi wa maswala ya mawasiliano na utangazaji ni “Uses and gratification theory”. (https://en.wikipedia.org/wiki/Uses_and_gratifications_theory unaeza chungulia hapa kujisomea zaidi kuihusu)

Kulingana na Elihu Katz (1974)msomi aliyevumbua na kuendekeza nadharia hii, licha ya wengi kuamini kwamba watazamaji na waskilizaji hupokea na kukubali chochote wanachopewa na vyombo vya radio na tv, ukweli uliothibitishwa ki-utafiti ni kwamba watengezaji na watayarishaji wa vipindi, huzingatia na kutilia maanani zaidi matakwa ya waskilizaji ama watazamaji wao.

Aidha ipo nadharia nyengine iliyovumbuliwa na Sandra Ball-Rokeach na Melvin DeFleur (1976) kwa jina “Media System Dependency Theory” (https://en.wikipedia.org/wiki/Media_system_dependency_theory unaeza chungulia hapa kujisomea ziadi kuihusu). Nadharia hii inaelezea ki-utafiti tabia ya binadamu kutegemea/kuchagua zaidi vyombo vya habari vinavyokidhi mahitaji yake ya habari,burudani n.k

Iwapo utafiti utaonyesha watu hupenda kitu flani wakati flani, utagundua vyombo vya habari hukimbilia na kuahakikisha hichi kinapatikana katika ule wakati unaotakikana, ndio mwishowe utaona kufanana kwa vipindi na idea katika vituo tofauti wakati mmoja wa siku.

Yote haya hua ni katika harakati za kutaka kumridhisha msikilizaji/matazamaji. Kumridhisha ili kumrai asalie nawe katika kipindi na kumbadilisha kuwa mfuasi wako sugu ama wa kipindi chako. Mwishowe mfuasi/msikilizaji huyu hutumiwa na watangazaji na wenye vituo kuwarai wanaotaka kutangaza bidhaa zao, kutangaza katika kipindi ama kituo husika, maanake hapo ndipo watapata waskilizaji wengi zaidi kwa wakati mmoja na kupata thamani ya fedha zao wanazotumia kulipia matangazo. Chunguza utagundua vipindi,vituo vinavyopendwa zaidi ama kuongoza kwa wingi wa mashabiki vimesheheni matangazo mengi sana, iwe kwenye tv ama radio.

Ni fahari ya kila mtangazaji kipindi chake kujaa commercial breaks, product activations, mentions etc sababu hii ni inshara moja wapo kwamba yeye ndio habari ya mjini. Inamaanisha anasikilizwa na wengi na ndio maana makapuni yanakimbia kutangaza katika kipindi chake, ili yapate thamani ya fedha za matangazo. Zaidi ya hapo muajiri wake naye hana budi bali kumuongezea mshahara mkubwa mtangazaji huyu ili kuhakikisha kwamba anasalia alipo na aendelee kumletea faida mithili ya mfugaji mwenye mifugo bora.

 

 

THE MOMENT OF TRUTH: Logo.©2007 FOX BROADCASTING

Ukweli

Huku wengi tukiwa wa haraka kuwaelekezea vidole vya lawama ma’Dj wanaocheza mziki wa kigeni, watangazaji wanaojaza playlist zao na mziki wa kigeni, ukweli unaofaaa kutopuuzwa ni kwamba wanachofanya ndicho kinachooitishwa na wengi zaidi. Huo mziki wa kigeni unaowaghasi baadhi ya washikadau ndio unaopendwa zaidi katika vilabu na majumbani mwa wengi. Mziki huo ndio uliojaa katika simu za wengi wetu. Ukweli urongo..?

Laiti leo klabu wimbo wa kigeni utachezwa na watu wasimame tisti na wasicheze lazima Dj atashtuka na kutafuta wimbo utakao ridhisha wale walisimama na kukataa kukatika. Lakini iwapo wimbo wa kigeni unatambulishwa na Dj na wengi wanashangilia na kupiga kelele, bila shaka huo wimbo utasalia katika playlist ya Dj na mtangazaji husika kila mara anapotafuta wimbo wa kucheza.

Laiti leo watu wataacha kuskiza vipindi sababu mziki unaochezwa ni wa kigeni, hakuna mtangazji atakayeshikilia tabia ya kucheza mziki wa kigeni. Kuna wakati huskiza simu za request katika vituo mbali mbali na husikitika sana kufuatia kiwango cha nyimbo za kigeni zinazoitishwa na wanaojiita waskilizaji sugu wa radio na mziki wetu wa pwani.

tech
Msikilizaji

Msikilizaji wa sasa wa radio ana uhuru mkubwa zaidi ikilinganishwa na msikilizaji wa zamani wakati hakukuepo na internet,smartphones n.k . Mziki wa kigeni kwa sasa unasambaa kwa uharaka zaidi miongoni mwa wasikiliazji kuliko hata miongoni mwa watanagazaji. Teknolojia imeleta urahisi wa watu kutumiana nyimbo mpya wanazopenda.

Mfano hai ni wiki iliyopita wakati kikundi cha Yamoto Band kiliachilia wimbo wake mpya kwa jina “Nigande.” Je wajua kwamba baada ya masaa manne katika mtandao, wasikilizaji wa radio yetu tayari walituma ujumbe mfupi kuitisha wimbo huu?

Sasa hapa mtangazaji hulazimika kudurusu mtandao kabla ya kugundua kwamba wimbo huu upo mtandaoni. Na ukweli, masaa sita baadaye blogspots, akaunti za kibinafsi za facebook za baadhi ya washikadau wa mziki wa kanda ya pwani zilisheheni taarifa kwamba wimbo mpya wa Yamoto umetoka Mistari iliyotoholewa kutoka kwa wimbo huu, ikiandamana na sifa kwa utunzi wa Yamoto Band ilisheni mitandao ya kijamii kwa siku kadhaa kiasi cha haja.

Sasa nani wa kulaumiwa hapa?

Watangazji tunaomba kuondelewa hichi kikombe cha lawama na kila mshikadau kuwajibikia wajibu wake kikamilifu iwapo tunataka kurekebisha hali iliyopo kwa sasa sababu miongoni mwa yanayotajwa kuwa suluhisho, lawama haipo katika orodha.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar