#PLAYKENYANMUSIC: PRODUCER NJE AWATAKA WAKENYA KUSHIKILIA HAPO HAPO!

0

Mtayarishaji wa mziki mkongwe kutoka kanda ya pwani Producer Nje wa record label ya Ufuoni Records International, amewapongeza Wakenya kwa kampeini yao ya katika mitandao ya kijamii, kushinikiza mziki wa wasanii wa Kenya kupewa kipau mbele katika vituo vya televisheni na radio nchini Kenya.

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa Facebook, Nje kwa njia ya moja kwa moja, amevitaka vituo vya radio na televisheni kucheza mziki wa Kenya bila ya ubaguzi wa misingi ya ujumbe wala umaarufu wa wasanii, ili kuhakiksiah tasnia ya mziki inakua nchini Kenya.

Producer Nje ambaye kwa sasa anaishi nchini Marekani, amewakumbusha Wapwani kwamba mapambano haya yalianza kitambo wakati mziki wa eneo la Mombasa ulipokua haupatiwi nafasi katika televisheni na radio jijini Nairobi, lakini baadhi ya mashabiki na watangazaji walipuuza lalama za wasanii.

Producer Nje ametaka mipaka ya kimziki idumishwe kuhakikisha tasnia ya mziki Kenya inanawiri na kuzaa faida kwa wasanii wa Kenya.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar