LEICESTER CITY YAPATA USHINDI WAKE WA KWANZA UEFA

0

Klabu ya Leicester City ya Uingereza jana ilishinda mechi yake ya kwanza katika kinyanganyiro cha kombe la UEFA, baada ya kuilaza Club Brugge ya Ubelgiji mabao 3 – 0 ugenini katika mechi ya kundi “G”.

Leicester ambayo ilikua inacheza ugenini ilipata mabao yake kupitia wachezaji Marc Albrighton na Riyadh Mahrez aliyefunga mabao mawili.

Mechi ya jana kwa Leicester ilikua ya 9 katika historia ya klabu hiyo na ushindi wa kwanza kwa klabu hiyo katika kinyanganyiro cha bara Uropa, tangu mwaka 1961.

Katika mechi nyengine ya kundi “G”.

Fc Porto ya Ureno imetoka sare ya bao 1 – 1 na wageni wao klabu ya Fc Copenhagen ya Uholanzi.

Sasa Klabu ya Leicester City imechukua uongozi wa kundi “G” ikiwa na jumla ya alama 3, Fc Copenhagen ya Uholanzi ni ya pili, Fc Porto ya Ureno niya tatu huku Club Brugge ya Ubelgiji ikishikilia mkia.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

Skip to toolbar