SWEDEN KUFANYIA RAIA WAKE UTAFITI WA NGONO

0

Serikali ya Sweden imeanzisha mpango wa utafiti kuchunguza mabadiliko ya tabia za raia wake, katika swala la kujihusisha katika tendo la  ngono.

Hii ni baada ya ripoti kudai kuwa wananchi wa taifa hilo hawajihusishi tena katika ngono kama ilivyokua miaka ya nyuma.

Waziri wa afya wa taifa hilo  Gabriel Wikstrom  amesema kupitia utafiti huo, wizara yake itaweza kuthibitisha kama ni kweli wananchi wa taifa hilo wamechoshwa na tendo la ngono kama inavyodaiwa.

435705-sex-new1

Sweden ni miongoni mwa mataifa tajiri ulimwenguni lakini linakabiliwa na upungufu wa idadi ya raia wake, kufuatia kupunga kwa idadi ya watoto wanaozaliwa.

Kulingana na serikali ya Sweden,utafiti sampuli hii ulifanywa mara ya mwisho miaka 20 iliyopita na hauezi kutumika tena, jambo lililopelekea kuanzishwa kwa utafiti mpya kutathmini hali halisi mashinani katika swala la ngono.

Comments

comments

About author

Teddy Mwanamgambo

Teddy Mwanamgambo is an On Air Personality/Producer @ Radio Kaya (93.1FmMsa,94.9FmVoi,99.7FmMlnd) Coast Kenya.

No comments

DIAMOND KUHAMIA KENYA

Msanii Diamond Platnumz kutoka nchini Tanzania amefichua kuwa anafikiria kuhamisha makao yake hadi nchini Kenya baada ya kujionea uungwaji mkono wa kiana yake na mashabiki ...
Skip to toolbar